DR MAGUFULI: Jembe la CCM na ahadi za kufufua viwanda









  Dr John Pombe Magufuli akiwa kwenye jukwaa wakati wa mchakato wa kunadi sera za chama za Mapinduzi akiomba ridhaa ya wananchi kuongoza nchi



 Na Voina Maganda
HESABU na uwezo wa kukariri unachangia kumtambulisha katika tasnia ya siasa, kila mwananchi utamsikia akisema jembe la hesabu, mzee wa namba, mzee wa kukariri, takwumu hizo na majina kadha wa kadha. Na hata alipomtambulisha mgombea mwenza alianza kwa hesabu ya uwiano wa 1:3 na hatimaye akaipata asilimia 66% huku akielezea sababu za kutumia hesabu hiyo, mwishoni akachanganua maana ya hesabu ile.

Umahiri huo sio wa kubahatisha bali ana utaalamu alioutafuta miaka kadhaa iliyopita na hali imemfanya akubalike kwa wananchi wengi pamoja na changamoto nyingi wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa majukumu yake.

Akiwa anafanya kazi katika wizara mbalimbali anatajwa kuwa kiongozi mwenye msimamo isiyotia shaka, hajui kuuma maneno lakini anajua nini anachokisimamia. Watendaji wa Wizara ya Miundombinu wanasema ni vigumu kumyumbisha Magufuli katika jambo ambalo anaona hilo ndiyo njia, lazima mlitekeleze kwanza. Tabia ya namna hiyo alikuwa nayo Mwalimu Julius Nyerere, kwamba akishaamua jambo kama anajua njia ya kupata muafaka wake, hukuna wa kumbadilisha.

Alipochagulia na kamati kuu ya chama chake kugombea nafasi hiyo alijitambulisha kwa wimbo wa kisukuma wa Alinselema Hadija na anaendelea kuutumia katika kampeni zinazoendelea.

Amewahi kushutumiwa kwa matukio kadhaa katika wizara alizofanyia kazi akiwa katika Serikali ya awamu ya tatu na nne kwa kuuza nyumba za serikali na kuisababishia serikali hasara kwa kulipa samaki waliosadikiwa kukamatwa katika mipaka ya Tanzania iliyoko ndani ya maji.

Ilikuwaje? Sina majibu ya hayo na hata kama ninayo siyo nia na jukumu langu kuyazungumzia, kwa kuzingatia msemo usemao “Bora kumuweka huru mwenye hatia kuliko kumfunga asiye na hatia,” msemo huu unampa nafasi aliye na shaka na jambo kufanya utafiti kabla ya kutoa maoni, huku tukitambua kuwa mahakama ndiyo ina wajibu wa kuhukumu baada ya kujiridhisha na ushahidi.





  Dr John Pombe Magufuli akiwa ofisini kwake kabla ya mchakato wa kuomba kura



Huyu ni Dk. John Magufuli  alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1959 wilayani Chato Mkoani Kagera (hivi sasa Chato ni wilaya ya mkoa mpya wa Geita) na atatimiza miaka 56 Oktoba mwaka huu.
Magufuli alianza elimu ya msingi Mwaka 1967 – 1978 Shule ya Msingi, Chato na baadaye Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
Alisoma sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza ambapo alihitimu mwaka 1978 na kujiunga  elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Juu ya Sekondari Mkwawa, Iringa.ambapo alihitimu 1981.
.
Baada ya hapo alijiunga na chuo Chuo CHA Mkwawa kwa ajili ya stashahada ya hisabati na kemia mpaka 1988.
Mwaka 1991 – 1994 alisoma shahada ya uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza, hakuishia hapo mwaka (2006 – 2009) alichukua Shahada ya Uzamivu ya Kemia  kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam..

Pamoja na kujituma katika elimu Magufuli ni shirika wa jeshi ambapo alihudhuria mafunzo katika kambi za Jeshi la kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma, JKT Makuyuni Arusha na  JKT  Makutupora, Dodoma.

Uamuzi wa Dk. Magufuli, kutangaza rasmi kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, haukuwa na mbwembwe tokea akichua fomu na hata aliporudisha na kusababisha kuwa kivutio zaidi kwa wadau wa siasa na hata kwa wafuasi wake ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

 Sasa ni jukumu lako mwamnanchi kuchagua kiongozi unayeona anakufaa kulingana na sifa za mgombea unayeamini kuwa atakuwa makini kwa manufaa ya Tanzania.

Hata hivyo, tofauti na Lowassa, Dk. Magufuli anatajwa kutokuwa na mizizi imara ndani ya CCM kwa vile hajawahi kuwa mjumbe katika vikao vya juu vya chama hicho, isipokuwa Mkutano Mkuu wa Taifa anaoingia kwa nafasi yake ya ubunge.

Dk. Magufuli, anajiamini na kusema kuwa anaomba ridhaa ya watanzania kupeperusha bendera ndani na nje ya mipaka ya Tanzania sababu ana sifa zote stahiki za kupiga na kupigiwa kura..

Dk. Magufuli amekuwa mbunge wa kuchaguliwa tangu mwaka 1995 na aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi; Wizara iliyokuwa ikiongozwa na Anna Abdallah.

Anajulikana kama kipenzi cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne, Benjamin Mkapa, ambaye mara kadhaa hakusita kumsifu hadharani, akimtaja kama mmoja wa ‘askari wa miavuli’ katika Baraza lake la Mawaziri.

Uwezo wake wa kukariri takwimu mbalimbali umekuwa kivutio kwenye mikutano mingi na kuwafanya watanzania wamuamini na kugundua anajua anachokifanya  hasa pale anapotoa taarifa za utendaji wa wizara alizoziongoza.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Ali Hassan Mwinyi, amewahi kumsifu kwa kumtaja kama ‘simba wa kazi’ kutokana na uchapa kazi wake katika wizara mbalimbali ambazo ameziongoza.

Kwa upande wa wananchi, wengi wanamuona Dk. Magufuli kama mmoja wa mawaziri wachapakazi waliowahi kutokea katika historia ya taifa letu.
  
Sasa anajinadi kwa kufufua viwanda ili kupunguza tatizo la ajira nchini, kuwawajibisha watu wanaotumia vibaya mali ya Umma na kwa manufaa yao maana anaamini kuwa chama chake kinaharibiwa na watu wachache wenye uchu wa mali na wasiojali maslahi ya taifa.

Magufuli hakuacha kuwataja wawekezaji wasio na dira ya maendeleo na kuahidi kurejesha uwekezaji huo na hatimaye kuwapa watu wenye uwezo nafasi ya kuwekeza.

Aidha amewaomba wananchi wasitafute muafaka wa matatizo yao kwa kuchagua raisi tofauti na yeye maana ataonyesha mabadiliko ndani ya siku mia moja za utawala wake iwapo watampa ridhaa ya kuongoza nchi.

Kazi alizowahi kufanya noi pamoja na:
Mwaka 2010 – hadi sasa Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).
Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)
Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.) Mwanza.
Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).
Amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi. Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa. Tofauti na wanasiasa wengine wengi, Dk. Magufuli ameandika vitabu na majarida mbalimbali ya kitaaluma. Ameoa na ana watoto kadhaa.

Comments